Historia ya ugunduzi wa bara la Amerika
.Anajulikana kama Christopher Columbus ni mzaliwa wa Spain kazaliwa mwaka 1451 na
kufariki 1504/6 akiwa na umri wa miaka 53 ni baharia maarufu sana katika historia na
wanafunzi wengi wanamtambia Chris kama mgunduzi wabara la American lakini Bado
hawaijui mpaka Leo ilikuwaje akagundua safari yake ilikuaje na yapi aliyo pitia kipindi yupo
njiani Leo tutayaona yotee . Ikumbukwe katika kipindi chote Hawa maabaria wanasafiri baharini hakukua na teknolojia
kama Leo walikuwa wakitumia merikebu (Mashua) ambazo zilikuwa zikiongozwa na upepo
tuu hivyo ili kuwa bahari ni lazima ujue majira ya mwaka vizuri na uelekea wa upepo ili
kuepukana na dhoruba wakati wasafari baharini. Napia Karne ya 15 kurudi nyuma watu wengi wa Ulaya, Afrika Amerika hakuna aliejua habari
kumuhusu mwenzie mpaka pale ubunifu wa vyombo vya majini ulipo gunduliwa , wapo
wanaosema wareno ndio Taifa la kwanza kugundua vyombo hivi vya majini . Na katika kipindi hiki chote habari zilizo kuwa zinajulikana ilikuwa ni uhindi ambapo
wafanya biashara walio wafanya biashara kati ya Ulaya na India walisimulia namna India ilivyo
tajiri na namna mfalme wa India anavyoishi anakula kwenye vyombo vya dhahabu, amevalia
mavazi ya dhahabu Pete na mapambo mengine mengi ya dhahabu . Basi hizo habari zilikuwa zina mtamanisha Kila mtuu atamani kufika huko India aonane na
huyo mfalme , kumbuka Ulaya katika kipindi hicho Cha Karne ya 15th walikuwa wapo kwenye
phase ya Bullion yaani kilikuwa na uhitaji mkubwa wa madini ya dhahabu, Shaba na fedha na
hiyo yote ni kutokana na walikuwa katika kipindi kutumia fedha kama njia ya biashara hivyo
walishatoka kwenye Barter trade system . Mfanyabiashara ambaye alijiingiza kwenye Hii
biashara ya kutafta haya madini alitajirika sana na hata ufalme ulitajirika pia. Basi bwana Chris na yeye alitamani sana kwenda huko na ikumbwe muda wote ule ulayala
hakuna aliye amini Dunia ni duara Kwani . Hivyo hakuna aliye amini ukipita njia kupika
magharibi unaweza fika India . Kwani kipindi hicho Ulaya ya kati kulitokea homa Kali ya Black death na kilikuwa na vita kati
ya waislamu na wakristu na vita hivyo vilidhaminiwa na papa yote haya yalifanya kuwe na
ugumu wa kufika huko India
Na Kwa kipindi hicho Nchi ya Ureno na Spain ndizo zilizo kuwa zimeendelea kiteknolojia
hasa za usafiri wa majini hivyo kulikuwa na ushindani baina ya nchi hizo mbili kwamba anaye
kuwa wakwanza kugundua maeneo mapya bas anaweka bendera yake na kutangaza kuwani
eneo lake na upaswi kumwingilia . Basi kilicho tokea ni Mfalme wa Spain na Ureno kutoa udhamini Kwa yeyote ataye weza
kutafta njia ya mpya ya kufika India Kwa upande wa Ureno ntaelezea siku nyingine Leo tupo
Spain. Basi mnamo mwaka 1492 August Mfalme alimpatia Columbus meli ndogo tatu na hapo
ndipo safari ilipo Anza kutoka bandari ya Spain iitwayo Palos . Zile meli Chris alizipa majina ya
kwake aliita Sanat maria akimaanisha maria mtakatifu na Zile mbili ziliitwa pinta na Nina. Kumbuka kabla ya safari Chris alionekana mwenda wazimu mabaharia wengi waliogopa
kusafiri naye hivyo Kwani hawakuamini kama safari inawezekana , basi siku tatu baadae meli
iitwayo pinta ilionekana usukani wake umelegea lakini ukweli ilikuwa mabaharia wawili lengo
ni safari ihairishwe na Chris arud nyumbani . Siku mbili baadae nahodha wa pinta
aliutengeneza lakini siku chache baadae uliharibika Tena hivyo Chris alilazimika kutia nanga
katika visiwa vya Canary ambavyo ni Mali ya Spain hivyo walitia nanga ili waweke usukani
mpya na ilitumika wiki tatu kukamilika Kwa usukani huo. Na usukuni ulikamilika na safariSasa hapo ndo ilikuwa safiri imeanza rasmi kwenye bahari isiyo julikana Kwanini waliita
hivyo kwasababu hakuna aliye wahi safiri kupitia uelekeo huo . Chris alihesabu maili na mail
pasipo kuwajulisha watu wake . Siku Moja wakati wapo njiani Kulikuwa na maradi sana lilipiga
Radio Kali kiasi kwamba mabaharia waoga walisemaa ni ishara ya wao warudi nyumbani
lakini Chris aliamuru wasonge mbele lakini siku kadhaa mbelen bahari ilikuwa shwari na meli
ilikuwa ikienda vizuri tuu pasipo shida Chris alifurahi sana Kwani watu walikuwa hawaaamini
kama Kuna upepo uvumao kupelekea Spain hivyo meli zilikuwa zikienda bila wasi wasi Wala
kugeuza matanga . Inakadiriwa kuwa ni majuma matatu tangu watoke kisiwa Cha canari ndipo asubuhi jua
lilipo chwaa nahodha wa pinta meli iliyo tangulia mbele alipaza sauti kuwa anaweza kuono
nchi kavu Kwa mbali . Chris kusikia hivyo alipiga magoti kumshukuru Mungu labda kwakuwa Chris alikuwa mtu
wa Mungu ndo maana alikuanaamini kuwa anaweza kufika na pia kulipa jina meli yake sanata
maria ni ishara Chris ni mcha Mungu , Kwa upande wa Nina Wao walipanda juu ya mlingoti
kujihakikishia nao pia waliweza sema wanaona nchi kavu . Basi kilicho fwata Chris aliamuru meli zote tatu zielekee upande ule wa nchi kavu usiku
kucha kulipo kucha jua lilipo toka chaajabu hawakuona kisiwa walichoona ni bahari tuu
kumbe Yale waliona ni mawingu ndio yaliwadanganya . Kumbuka Mfalme wa Spain alihaidi kumpatia zawadi yeyote atayekuwa wakwanza kuona
nchi kavu hivyo ilikuwa ni kama mchezo wa maahindano meli ya Nina ndiyo iliyo kuwa mbele
ya msafara hivyo mabaharia wake walikuwa na matumain kupata tuzo hiyo ya mfalme . Basi
siku chache baadae meli ya Nina ilipiga mzinga kuasharia Kuna kisiwa mbele lakini haikuwa
kweli macho yaliwadanganya . Naweza kusema hamu waliyo kuwa nayo ya kutaka kuwa
wakwanza kuona nchi kavu ndo iliyo wasababisha waone Kila kitu ni nchi kavu kumbe
mawingu. Wale mabaharia walighairi na kukata tamaa ya kupendelea na safari. Lakini Chris
aliwapamoyo na kumtanguliza Mungu mbele . Asubuhi yake walipo amka waliona ndege aina ya vitwitwi na kuangalia baharini vizuri
waliona Jani hivyo niishara kuwa kisiwa hakipo mbali ilipo fika saa nane usisu Chris aliona
kwambali aliona kitu kama mwanga unawaka na kuazima mwanga kama wa mshumaa ndipo
alipo amuru meli zote zisimame na kungja Hadi kesho palipo kucha waliona Mchanga wa
bahari 😳 ilikuwa mshangao na furaha isiyo na kifani waliona wakati wanakarbia waliona
wenyeji wanakuja Kwa Kasi huku wakiwa wanakuja kushangaa meli na hapo ni wiki kumi
tangu walipo toka canary na Chris aliamuru kutia nanga walipo fika Cha kwanza waliweka
mlingoti wa bendera ya mfalme wa Spain kuasharia hicho ni kisiwa Cha Spain Chris alikiita
San Salvador maana yake ikiwa mwokozi mtakatifu na hiyo ni kutokana na kuwa walikuwa
washa katatamaa. Waliposhuka wenyeji walikimbiaa lakini baada ya muda walirudi na ndipo Chris akawapa
zawadi Kofia, njuga,shanga na vibumba vya Uzi wa Kamba wenyeji walifurahi sana pia
waliona kama Chris Amerika mbinguni kutokana na mavazi waliyo vaa na rangi Yao nyeupe . Ndipo Chris lipo andika kitabuni
Kuwa wenyeji hao hutembea uchi kabisa maumbo yao ni mazuri na sura zao pia ni nzuri
rangi Yao ni weusi kama wale wa visiwa vya Canary , anaendelea kuandika wengine hujipaka
rangi nyekundu wengine nyeupo wengine hujipaka mwili mzima wengine puani wengine
machoni . Wakati wapo kambini mmoja wa wale wenyeji alaishika upanga akajikata Kwani
alikuwa hajui kisu au panga kama kinaweza mkata , wanatumia mitumbwi kusafiria majini
mitumbwi hiyo inaweza kubeba Hadi watu 40 mingine midi ya mtu mmoja hutumia kifaa
kama mwiko mkubwa kuendeshea . Bahati mbaya Chris lipo watazama aliona baadhi Yao wamejichoma Pini ya dhahabu puani
na ndipo alipoona kuwa sasa amefika Kwa yele mfalme tajiri atumiaye glass ya dhahabu namakombe mengine . Kumbe yupo kwenye sehemu ya bara kubwa Lilo julikana lakini baada ya watu kupata habari
zake alikiita American ndo mpaka sasa linaitwa hivyo . Chris alikuwa na hamu sana ya kujua na kumuona mfalme huyo ambaye habari zake
amekuwaa akizisikia Kwa muda pasi kujua amegundua njia ya kwenda bara jipya lisilo
julikana ndipo alipoanza safari ya kuondoa kisiwani hapo maana alikwishwa gundua hapo
sio India Chris aligundua visiwa vingi kama Fernandina kisiwa kilicho pewa jina la mfalme wa
Spain na kisiwa Cha Isabella Kwa heshima ya malkia vingi aliviita juani jina la mtoto wa
mfalme Kisiwa hicho Cha juani sasa ndio linaitwa Cuba mpaka sasa jina lake ndo Hilo
ikumbukwe Chris wakati anaondoka aliondoka na wenyeji wa San Salvador ili wawaelekeze
njia wenyeji hao walikuwa wakiwaogopa jamii ya watu walio waita Caribs ambao wao ni
desturi Yao kula nyama za watu . Chris hakubahatika kuona dhahabu ila alikutana na viungo vya vyakula vingi pia wenyeji hao
walikuwa wakivutaa majani ambayo kwasasa yanaitwa Tumbaku . Walikaa kwa muda kidogo walilo ondoka walifika katika kisiwa Cha Haiti na ilikuwa ni siku
ya kuzaliwa yesu krismass . Alikuwa amechoka sana usiku ule ilimbidi apumzike Kwani hakulala siku mbili basi
alikwenda kulala Kwa sababu bahari ilikuwa shwari kazi ya kuongoza chombo alimwachia
mtoto usukani , ilipo fika usiku wa manane meli Ile ili kokotwa na mkondo waa maji ikakwama
mchangani . Kuona vile yule mtoto akapiga kelele Chris kusikia vile akaamka na kwenda juu
alimwamrisha nahodha wa Ile meli nyingine aikwamue Kwa kuivuta meli Ile kutoka
mchangani . Lakini chaajabu wale watu badala ya kutii amri walikimbiaa mail Moja. Ili
waokokoke walikimbiaa kuelekea upande wa meli ya Nina lakini yule nahodha aliwarudisha
kurudi ili wasaidiane kuikwamua Ile meli. Ilimpasa apakue Sheena yote iliyopo kwenye meli ili ipungue uzito na mfalme wa kisiwa kile
alipeleka watu wamsaidie kuikwamua meli Ile na kupakua Shehena ile. Sasa Columbus alikuwa na meli Moja tuu Nina hivyo ili mpasa awaache baadhi ya watu ili
arudi San Salvador na wale wenyeji ili akamuonejeshe mfalme na malkia wa Spain. Kwani meli yake isinge kwama basi asinge waacha hapo basi Columbus aliwaamuru
wajenge mnara mrefu na ngome Ile wapate usalama wapo kisiwani hapo.kabla ajaondoka
walipata chakula Cha pamoja kabla ajaondoka aliwaambia watu wake wanao baki watakuwa
watu wema kwao na kuwalinda dhidi ya adui zao Caribs ikiwa watakuja kuwashambulia . Basi
bwana akipiga mzinga mmoja juu watu walio kuwepo karibu wakainama chini. Chris akaamua
wafanye mchezo wa vita lengo ni watu wale wanaobaki pale waone wale ni marafiki zao na
hivyo walifundishwa mbinu za kujihami na Caribs . Wakati anaondoka alipita katika visiwa mbalimbali ambavyo hawakuwa kuviona hapo kabla
nakimoja wapo aliwashusha wapate kula viazi vikuu walipo shuka kumbe Kulikuwa na zaidi ya
watu 50 wamejificha katikati ya miti wakiwa na Sila Columbus na wenzake walitia nanga na
walipo fika waliomba kufanya biashara wabadilishane silaha za wenyeji na shanga lakini
wenyeji waliuza silaha mbili tuu na walikataa kuuza zaidi ya hapo ukatokea ugomvi watu wa
Chris wakamjeruh Mwenyezi wakakimbia. Chris alichukia kitendo hicho Cha kuwajeruhi
wenyeji Kwani hakupenda kugombana na wenyeji wake
Basi lakini walidha wale watakuwa ni Caribs na kama watakuwa ni wao basi watakuwa
wamewapa funzo ili wawaogope watu wa Spain , Columbus akukaa sana akafinga safari
akaanza kuondoka laki meli ya Pinta ilikuwa imeharibika kidogo mlingoti wake na
hawakuweza kuweka nanga hivyo meli ya Nina ilibidi kuwa ngoja Kila mara Kwa mara. Ilikuwa ni mwezi februari ambapo bahari ilikuwa imechafukwa meli zile naddoruba Kali Columbus aliogopa Sana aliona kama wanaenda kufaa , hivyo aliandika
waraka kwenye ngozi na kupitia nta ili usiloane na aliuweka kwenye chupa ya mtu na kuitupia
baharini ili Kwa yeyote ataye uona aweze kumtaarifu mfalme wa Spain . Hatimaye Nina ikifika visiwa vya Azores ambavyo ni chini ya imaya ya wareno na akatulia
mpaka dhoruba ilipo isha na akaanza safari upya Kwa muda wa siku mbili bahari ilikuwa
shwari lakini baada ya hapo upepo ukaanza kuvuna Tena mpaka matanga ya meli ya Nina
yaka tatuliwa vibaya dhoruba iliambatana na radi Kali , na dhoruba hiyo ilidumu ndani ya siku
Saba ndipo walipo fika nchi ya Ureno . Na alipumzika Ureno Kwa muda wa wiki Moja na kuikarabati meli yake Tena lakini Chris
anadai kuwa hajawahi kuona dhoruba Kali kama hiyo tangia aanze ubaharia wake na ni
maajabu kupona kwake ndipo alianza safari kutokea Ureno kuelekea kwao Spain Ndipo alipo
fika bandalin ya Palos alipoanza safari Spain kumbuka mwaka mzima ulikuwa umeisha. Kwa upande wa Spain Kulikuwa ni furaha sana Kila mtu alifurahia kumuona Columbus
amerejea na mfalme kusikia taarifa hizo Ali mwalika katika kasri lake akapate karamu nae
alikuwa kaja na zawadi nyingi sana Viazi, dhahabu, kasuku, mimea mingine migeni , jambo
jingine wa Spain alifurahi sana kuwaona wale wageni walio ambatana na Columbus ambao
aliwachukua kutoka huko katika visiwa alivyo pita . Kuanzia hapo watu wengi walitamani kusafiri na Columbus ili wazione nchi alizo zigundua
huko alipo toka , inadaiwa alisafiri mara tatu na aliona mambo mengi zaidi na yaajabu , lakini
SI Kila mtu ataweza furahia mafanikio Yako Kuna ambao walimwonea wivu na kumpelekea
mfalme na malkia habari za uongo . Kuna hata siku Moja walirejea na mfungwa kafungwa
minyororo mfalme na malkia wali huzunika kuona vile lakini hizo zote ni figisu za kumchafua
Chris . Tangia Chris agundue hizo nchi mpya hakuishi Tena maisha ya furaha kwasababu
watu Hawa kumpenda sababu ya wivu. Chris hakuwahi kufika India katika maisha yake yote mpaka anafariki mwaka 1504/6 lakini
aliacha mchango mkubwa wakugundua bara kubwa ambalo waliliita "new world" (Dunia mpya)
na kumbuka alifa kwenye bara Hilo kibati mbaya yeye alitamani kufika India hivyo kufika huko
alidhani yupo India ndo maaana wenyeji wake aliwaita west indies yaani uhindi wa magharibi .