Michezo

 

Uhamisho wa Kylian Mbappe: Je, atakwenda Saudi Arabia au Real Madrid ? 



Maelezo ya pic


Mustakabali wa Kylian Mbappe umekuwa sakata la uhamisho wa majira ya kiangazi.

Huku nahodha huyo wa Ufaransa akikataa kusaini mkataba wa kuongeza muda katika klabu ya Paris St-Germain. Mabingwa hao wa Ufaransa wanajaribu kupata saini ya mfungaji huyo bora ili kuepuka kumpoteza msimu ujao.

Klabu ya Al-Hilal ya Saudi Arabia, ilishangaza ulimwengu wa soka siku ya Jumatatu kwa kuweka dau la rekodi ya dunia la pauni milioni 259. Je, anaweza kubadilisha Ligi na kwenda Ligi Kuu ya Saudia?

Tumefikaje hapa?

Mbappe, alijiunga na PSG mwaka wa 2017, awali kwa mkopo kutoka Monaco kabla ya uhamisho wa euro milioni 180 (pauni milioni 166), amefunga mabao 212 katika michezo 260.Licha ya mafanikio mengi ya ndani na kuunda kikosi cha washambuliaji wakiwemo nyota watatu wakubwa duniani Mbappe, Neymar na Lionel Messi, klabu hiyo inayomilikiwa na Qatar imeshindwa kufikia lengo lao kuu la kushinda Ligi ya Mabingwa.

Mbappe ana mkataba hadi Juni 2024, lakini mwezi uliopita ilibainika kuwa aliiambia klabu kuwa atasalia msimu huu lakini hataongeza mkataba wake. Mgogoro huo umekuwa mchungu, huku PSG wakimwacha nje Mbappe katika ziara yao nchini Japan na Korea Kusini ya kujiandaa na msimu mpya

Katika mchezo wao wa kwanza katika ziara hiyo, PSG walitoka sare ya 0-0 na timu nyingine ya Saudi, Al-Nassr, mjini Osaka, Japan.

"Kylian Mbappe ni mchezaji mzuri na hayupo," mlinzi wa PSG Danilo Pereira alisema baadaye. "Huo ni uamuzi wa klabu, siwezi kuzungumzia chochote."

Atakwenda Saudi Arabia? 


Maele





wenyekiti wa PSG, Nasser Al-Khelaifi ameweka wait dhamira yake ya kuchukua msimamo mkali na kumekuwa na mapendekezo kwamba Mbappe hatachaguliwa kwa mwaka mzima iwapo atakataa kuvunja mkwamo uliopo.

Klabu hiyo ya Ufaransa sasa imeipa Al-Hilal, mojawapo ya klabu nne zinazomilikiwa na Mfuko wa Uwekezaji wa Umma wa Saudi Arabia, ruhusa ya kuzungumza na Mbappe. PSG wanatarajia vilabu vya Ulaya kuwasilisha maombi pia.

Mwandishi wa habari wa soka wa Ufaransa Lisa Leroux anaamini ofa ya pauni milioni 259 inathibitisha Mbappe "kweli ni mchezaji bora wa kizazi chake."

Iwapo atahamia Saudia, huenda Mbappe akawa mchezaji anayelipwa pesa nyingi zaidi katika kandanda, akipata kiasi cha pauni milioni 177 kila mwaka, ambacho nahodha wa Ureno Cristiano Ronaldo alikipata katika klabu ya Al Nassr baada ya kuhama kutoka Manchester United mwezi Disemba.

"Hakuna mchezaji aliyewahi kupewa mshahara huu katika soka, na nadhani hata katika historia ya michezo kwa mwaka mmoja," Leroux anasema.

"Mshahara ambao atapata utakuwa wa kihistoria na nje ya ulimwengu huu. Itakuwa kama euro milioni 59 kwa mwezi, karibu euro milioni 2 kwa siku."

Mtaalamu wa soka wa Ufaransa Julien Laurens anaamini Mbappe hatakwenda Saudia.

"Hataki kwenda huko," Laurens aliambia BBC. "PSG inaposema tumetoa ruhusa ya kuzungumza na Mbappe, hataki kuzungumza nao, Al-Hilal wanafahamu hilo sio kuhusu pesa.’’

"Anataka tu kushinda kila kombe linalowezekana. Hivi sasa, akiwa na umri wa miaka 24, hiyo haijumuishi Ligi ya Saudia."

Ama atakwenda Real Madrid?


Laurens anafikiri Real inapaswa kumchukua Mbappe msimu huu wa joto, badala ya kusubiri hadi awe huru, na kuingia kwenye vita vya zabuni.

"Kama watamsajili sasa basi timu yao itakuwa bora zaidi. Kwa nini wasubiri kama wana pesa?" aliongeza.

Je, mchezo wa haki za kifedha unatumika kwa Saudia?

Mnamo Juni, vilabu vinne vikubwa nchini humo vya Al-Ittihad, Al-Nassr, Al-Hilal na Al-Ahli, vilichukuliwa na Mfuko wa Uwekezaji wa Umma wa nchi hiyo, ambao pia unamiliki Newcastle United.

Tangu Ronaldo asajiliwe, timu 18 za ligi hiyo zimeingia kwenye matumizi makubwa ya fedha na kuwavutia baadhi ya vigogo wa mchezo huo kutoka Ulaya wakiwemo Karim Benzema, N'Golo Kante na Ruben Neves, huku nahodha wa Liverpool, Jordan Henderson akihusishwa kutaka kusajiliwa.

Vilabu vya kandanda vya Ulaya vinapaswa kuzingatia kanuni za kifedha zinazojulikana kama Financial Fair Play, ili kuhakikisha kuwa vilabu havitumii pesa zaidi ya zinazopata.

Lakini hii haitumiki kwa Saudi Arabia, ambayo iko katika Shirikisho la Soka la Asia, anasema mtaalamu wa fedha wa soka Kieran Maguire.

"Kinachotofautisha Ligi Kuu ya Saudia na soka ya Ulaya ni kwamba hakuna kizuizi cha haki za kifedha," alisema.

"Kwa hivyo, hata kama vilabu vya Premier League vitatoa pesa zaidi, siku zote vitashindwa kwani [vilabu vya Saudia] havina vikwazo vyovyote vya kudhibiti gharama."

Chanzo

BBC

Previous Post Next Post

No Thumbnail

News app yako bomba sasa unaweza idownload kwa kubonyeza batani ya download hapa ,