Je dawa za Antibiotics zina madhara kiafya?

mageuzi na baiolojia katika Chuo Kikuu cha Oxford. "Bakteria sugu wanaweza kuhama kutoka kwenye utumbo hadi maeneo mengine, hivyo kinachotokea kwenye utumbo kina athari kwa mwili wetu wote," anasema.

f

CHANZO CHA PICHA,

GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Wanasayansi wanasema matumizi ya kiholela ya antibiotiki yanaweza kuwa na athari za muda mrefu kwa afya ya utumbo na mfumo mpana wa kinga

Athari mbaya na za kuokoa maisha za antibiotiki ni moja ya utata mkubwa unaowasumbua wanasayansi kote ulimwenguni.

Ingawa hakuna suluhu moja, kuna mbinu ambazo zinaweza kupunguza madhara ya antibiotics kwa afya zetu.

"antibiotics ni dawa za ajabu ambazo zimeokoa mamilioni ya maisha. Ni rasilimali za thamani sana na zinapaswa kutumiwa, lakini tunahitaji kuelewa jinsi ya kuzilenga kwa usahihi," anasema Kinross.

Wanasayansi sasa wanaangalia antibiotiki zinazolenga zaidi sehemu za mwili, na vile vile zinazolenga bakteria maalum, MacLean anasema, kwa wazo la kuondoa tu bakteria unayotaka kuondoa, na kuacha bakteria yenye faida ndani ya utumbo mzima.

Lakini chombo kikubwa zaidi tulicho nacho kwa sasa, anasema Anthony Buckley, profesa mshiriki katika baiolojia ya utumbo katika Chuo Kikuu cha Leeds, ni mlo wetu. "Lishe ni mojawapo ya vichochezi vikubwa katika kutengeneza mfumo wa bakteria katika binadamu," anasema.

Kikundi cha utafiti wa maambukizo yanayohusiana na afya cha Chuo Kikuu cha Leeds kimekuwa kikijaribu athari za antibiotics kwa bakteria wazuri wa utumbo kwa miongo miwili iliyopita.

Ni bora zaidi kutotegemea antibiotiki - James Kinross

Aina nyingi zaidi za vyakula tunavyokula kawaida huhusishwa na aina nyingi za vijidudu kwenye utumbo, na nyuzinyuzi haswa zinaonekana kuwa na athari chanya, "anasema Ines Moura, mtafiti mwenza katika kitivo cha dawa na afya cha Chuo Kikuu cha Leeds, ambaye kwa sasa anafanyia majaribio ya athari za virutubishi tofauti kwenye mfumo wa bakteria wa utumbo na jinsi unavyoweza kupunguza athari mbaya za antibiotiki.

Nyuzinyuzi za lishe ni muhimu sana kwa sababu vijidudu katika mwili wetu huzimeng'enya na kutoa asidi fupi ya mafuta, ambayo hutoa nishati kwa seli zinazozunguka utumbo, anasema Buckley.

"Unapokuwa na antibiotiki, vijidudu vinavyozalisha asidi ya mafuta ya utumbo mfupi hupungua na kuchukua muda kupona. Nadharia yetu ni kwamba, kwa kumeza nyuzinyuzi za chakula, hutoa utumbo unaweza kuwezesha kutengenezwa kwa bakteria hizo na kuzikuza na kuzalisha asidi ya mafuta, na hivyo kunakuwa na matumaini ya kuweka usawa wa bakteria tena kwenye utumbo, "anasema.

h

CHANZO CHA PICHA,

GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Kula lishe yenye nyuzinyuzi nyingi hufikiriwa kusaidia kuunda mazingira ya utumbo yenye manufaa zaidi kwa bakteria yenye afya

Ajabu inayotokana na utumiaji wa antibiotiki ni kwamba, kwa kila dozi tunayotumia, tunaweza kupunguza uwezo wa miili yetu kupigana na maambukizo, na kwa hivyo kuongeza utegemezi wetu kwa dawa hizo.

"Ni bora zaidi kutotegemea antibiotiki," Kinross anasema, "Na badala yake kuzingatia ustahimilivu wa kibaolojia wa ikolojia yetu ya ndani kwa kula vyakula vyenye virutubisho na vyenye kuleta afya, haswa katika maisha ya mapema ya mtu, kwani wakati huu ndio wakati ambapo antibiotics husababisha uharibifu mkubwa. "

Chanzo BBC

Previous Post Next Post

No Thumbnail

News app yako bomba sasa unaweza idownload kwa kubonyeza batani ya download hapa ,