Vita vya Israel na Hamas: Jeshi la Israel lakamilisha maandalizi ya kuwapokea mateka



Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) linasema maandalizi ya kuwapokea mateka yamekamilika.

Katika sasisho kwenye mitandao ya kijamii, IDF inasema maeneo kadhaa yametayarishwa kwa ajili ya kuwapokea , ikiwa ni pamoja na msaada wa matibabu.

Baada ya mapokezi na matibabu yoyote ya awali, mateka watahamishiwa katika hospitali katika maeneo mengine nchini Israeli ili kuunganishwa na familia zao.

IDF pia limechapisha , zikiwemo picha za eneo la kuchezea lililowekwa kwa ajili ya watoto, mifuko ya kile kinachoonekana kuwa ni matibabu au vifaa vingine vya kibinadamu na helikopta ya kijeshi ya kuwabeba mateka hao wanaoshikiliwa na Hamas tangu ilipofanya mashambulio dhidi ya Israel.

Chanzo BBC


Previous Post Next Post

No Thumbnail

News app yako bomba sasa unaweza idownload kwa kubonyeza batani ya download hapa ,