Siasa



UWT WAWATAKA WENYE KUUTAMANI URAIS ZANZIBAR 2025 WAMWACHIE DK.MWINYI.


Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amewashukuru viongozi wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) kwa kuthamini kuandaa mkutano uliojumuisha Wanawake kutoka sehemu mbalimbali nchini ikiwemo  mikoa yote ya Tanzania bara.

Dk.Mwinyi amesema hayo  katika mkutano wa kumpongeza kutimiza miaka mitatu ya uongozi wake ulioandaliwa na Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) uliofanyika viwanja vya Maisara Mkoa wa Mjini Magharibi leo tarehe 04 Novemba 2023.

Aidha, Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania bara Abdulrahman Kinana ampongeza Rais Dk.Mwinyi kwa kuimarisha umoja, mshikamano na utulivu wa nchi na kuwaletea maendeleo Wazanzibari.



 Amesema katika miaka miwili iliyobaki utekelezaji wa miradi ya maendeleo utakuwa mkubwa zaidi na Zanzibar baada ya miaka 10 itakuwa ya maendeleo makubwa. 

Naye, Mwenyekiti wa UWT Taifa Mary Chatanda amesema UWT wameridhika na utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya mwaka 2020/2025 kwa kuvuka malengo ya utekelezaji ndani ya miaka mitatu kwa miradi mbalimbali ya maendeleo iliyotekelezwa Zanzibar .

Vilevile ameeleza kuwa UWT watamchukulia na kumjazia fomu ya kuomba Urais wa Zanzibar  Dk.Mwinyi pia watafanya hivyohivyo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dk Samia Suluhu Hassan  mwaka 2025.

🗓️04 Novemba 2023

📍Viwanja vya Maisara, Mkoa wa Mjini Magharibi.
Previous Post Next Post

No Thumbnail

News app yako bomba sasa unaweza idownload kwa kubonyeza batani ya download hapa ,