Trending

Kiongozi wa kanisa katoliki Papa Fransis aashiria kuunga mkono ndoa za jinsia moja. 

Watu waliobadili jinsia wanaweza kuwa wazazi wa ubatizo katika Kanisa Katoliki, mashahidi katika harusi za kidini na kubatizwa , ofisi ya mafundisho ya Vatikani ilisema Jumatano, ikijibu maswali kutoka kwa askofu.
Idara hiyo, inayojulikana kama Dicastery of the Doctrine of the Faith, haikuwa wazi hata hivyo, katika kujibu swali la ikiwa wenzi wa jinsia moja wanaweza kuruhusiwa kupata ubatizo wa Kanisa kwa ajili ya mtoto aliyeasiliwa au ule uliopatikana kupitia mama mlezi.
Askofu Jose Negri wa Santo Amaro nchini Brazili alituma kwa ofisi ya mafundisho maswali sita mnamo Julai kuhusu watu wapenzi wa jinsia moja na waliobadili jinsia (LGBT ) na ushiriki wao katika sakramenti za ubatizo na ndoa.

Kurasa hizo tatu za maswali na majibu zilitiwa saini na mkuu wa idara hiyo, Kadinali wa Argentina Víctor Manuel Fernández, na kuidhinishwa na Papa Francis mnamo Oktoba 31.

Ziliwekwa kwenye tovuti ya idara hiyo Jumatano kwa kutumia neno la Kiitaliano "transsexuals".

Francis, mwenye umri wa miaka 86, amejaribu kulifanya Kanisa liwe na ukarimu zaidi kwa watu wa jumuiya ya LGBT bila kubadili mafundisho ya Kanisa, ikiwa ni pamoja na msemo mmoja kwamba kuvutia watu wa jinsia moja si dhambi bali ni dhambi ni kitendo chenyewe cha kushiriki mapenzi ya jinsi moja.

Katika kujibu swali la kama watu waliobadili jinsia wanaweza kubatizwa, ofisi ya mafundisho ilisema wanaweza kwa masharti fulani na mradi tu "hakuna hatari ya kusababisha kashfa ya umma au kuchanganyikiwa miongoni mwa waumini".

chanzo BBC
Previous Post Next Post

No Thumbnail

News app yako bomba sasa unaweza idownload kwa kubonyeza batani ya download hapa ,