Vikosi vya Al Quds vyasema vipo tayari kuwaachia mateka wawil


Vikosi vya Al-Quds, tawi la kijeshi la harakati ya Jihad ya Kiislamu ya Palestina (PIJ) ilitangaza katika taarifa hapo jana (Alhamisi) kwamba iko tayari kuwaachilia mateka wawili kwa sababu za kibinadamu.

Taarifa hiyo kwa Kiarabu iliwataja mateka hao wawili kuwa ni "Hanna Katsir na mvulana Yagil Yaqoub," bila kutaja mataifa yao.

Mpango huo utatekelezwa ikiwa masharti fulani yatatimizwa ili kuhakikisha usalama wa watu wa Palestina, taarifa hiyo iliongeza.

Mapema siku hiyo, chanzo cha serikali ya Israel kiliiambia Xinhua kwamba Israel iko "tayari" kusitisha mapigano kwa muda katika Ukanda wa Gaza ikiwa Hamas itaonyesha "dhamira ya kweli" ya kuwaachilia mateka.

Wizara ya afya huko Gaza ilisema Alhamisi kwamba idadi ya vifo vya Wapalestina kutokana na mashambulizi ya Israel kwenye eneo la Palestina ambayo imekuwa ikiendelea kwa zaidi ya mwezi mmoja iliongezeka hadi 10,818.

Operesheni za kijeshi za Israel zilikuja kulipiza kisasi kwa mashambulizi yaliyoongozwa na Hamas mnamo Oktoba 7, ambapo zaidi ya watu 1,400 waliuawa nchini Israeli na karibu mateka 240 walichukuliwa, kulingana na takwimu za Israeli.
Chanzo 
China Xinhua News
Previous Post Next Post

No Thumbnail

News app yako bomba sasa unaweza idownload kwa kubonyeza batani ya download hapa ,