NAMNA AKILI BANDIA INAVYO TUMIWA KUGUNDUA MATATIZO YA MOYO

chuwaz.com


Akili Mnemba (AI) inaweza kutumika kutambua wagonjwa walio katika hatari ya kushindwa kwa moyo, ikimaanisha kuwa wanaweza kutibiwa mapema, watafiti wa Leeds wamesema.

Algorithm, inayojulikana kama Find-HF, "imefunzwa" na watafiti wa Chuo Kikuu cha Leeds kugundua dalili za mapema za hali hiyo kwa kutumia rekodi za wagonjwa.

Kulingana na Wakfu wa Moyo wa Uingereza (BHF), kwa sasa kuna zaidi ya watu milioni moja nchini Uingereza wenye matatizo ya moyo.

Prof Chris Gale, kutoka Leeds Teaching Hospitals NHS Trust na Chuo Kikuu cha Leeds, alisema teknolojia hiyo itafungua "fursa muhimu" kwa wagonjwa.

Kwa utafiti huo, ambao ulifadhiliwa na BHF, watafiti walitumia rekodi za wagonjwa wa watu wazima 565,284 wa Uingereza kutoa mafunzo kwa algorithm ya AI,

Kisha ilijaribiwa zaidi kwenye hifadhidata ya rekodi 106,026 kutoka Hospitali ya Chuo Kikuu cha Kitaifa cha Taiwan.

AI iliweza kutabiri kwa usahihi wagonjwa walio katika hatari kubwa zaidi ya kupata ugonjwa wa moyo, na wale ambao wangeweza kulazwa hospitalini na hali hiyo, ndani ya miaka mitano, watafiti walisema.

Chanzo

BBC Swahili

Previous Post Next Post

No Thumbnail

News app yako bomba sasa unaweza idownload kwa kubonyeza batani ya download hapa ,