CHOMBO CHA CHINA KILICHONENDA MWEZINI CHAANZA SAFARI ZA KUEREJEA DUNIANK

chuwaz.com


China inasema ujumbe wake umeanza kuondoka upande wa mbali wa mwezi kurejea Duniani ukiwa umebeba sampuli za kwanza kabisa zilizokusanywa kutoka eneo hilo.

Vyombo vya habari vya serikali vinasema sehemu ya chombo cha Chang'e-6, iliyopewa jina la mungu wa kike wa mwezi katika elimu ya mambo ya asili ya Kichina, kilifanikiwa kuondoka salama kuanza safari ya kurejea mnamo saa 07:38 siku ya Jumanne (23:38 GMT Jumatatu).

Chombo hicho kilitua Jumapili karibu na ncha ya kusini ya mwezi katika hafla ya kwanza ya ulimwengu iliyoadhimishwa na jumuiya ya kimataifa ya sayansi.

China ndio nchi pekee iliyotua upande wa mbali wa mwezi, baada ya kufanya hivyo hapo awali mnamo 2019.

Utawala wa Kitaifa wa Anga za Juu wa China umeita tukio hilo ''jambo lisilokuwa la kawaida katika uchunguzi wa mwezi na binadamu''.

Upande huo wa mwezi - ambao daima hutazamana mbali na Dunia - ni changamoto kufikia kutokana na ardhi yake na mashimo ya kina kirefu.

Ujumbe wa China unalenga kuwa wa kwanza kurejesha sampuli za mawe na udongo kutoka eneo hilo, ambazo wanasayansi wanasema zinaweza kuwa tofauti sana na miamba iliyo karibu na mwezi.

Vyombo vya habari vya serikali vilichapisha video kutoka sehemu ya anga za juu ya China zikionyesha chombo husika kikipeperusha bendera ya China baada ya kukusanya sampuli hizo za thamani.

Chanzo 

BBC Swahili

Previous Post Next Post

No Thumbnail

News app yako bomba sasa unaweza idownload kwa kubonyeza batani ya download hapa ,