NETANYAU APUUZA AGIZO LA KUSITISHA VITA DHIDI YA HAMAS

chuwaz.com


Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu Jumatatu alipuuza matarajio ya sitisho la mara moja la mapigano katika vita dhidi ya Hamas huko Gaza, akisema kwamba mpango uliopendekezwa na Rais Joe Biden wa kusitisha mapigano na kuachilia mateka wanaoshikiliwa na Hamas umezungumzia baadhi ya masuala.

Netanyahu kwa muda mrefu amekuwa akishinikiza kutokomezwa kwa Hamas huko Gaza, lakini alisema katika taarifa,” Madai kwamba tumekubali sitisho la mapigano bila masharti sio sahihi.”

Biden alielezea mpango mpya wa sitisho la mapigano huko Gaza wiki iliyopita ambao unajumuisha kusitishwa kwa mapigano na kuachiliwa kwa baadhi ya mateka wanaoshikiliwa na Hamas.

Hata kama maafisa wa Israel wametilia mashaka yaliomo katika pendekezo hilo la kusitisha mapigano, jeshi limetangaza kwamba mateka wengine wanne waliotekwa nyara na Hamas sasa wamethibitishwa kuwa wamekufa, wakiwemo wazee tatu walioomba bila mafanikio watekaji wao wa Hamas kuwaachilia.

Maafisa wa Marekani wanasema wanaamini ikiwa Hamas itakubaliana na pendekezo hilo la kusitisha mapigano, jambo ambalo bado haijafanya, basi Israel itakubali pia.

Msemaji wa serikali ya Israel alisema kwamba “vita vitasitishwa kwa masharti ya kuwaachilia mateka” baada ya hapo mazungumzo yataendelea juu ya jinsi ya kufikia lengo la vita vya kuitokomeza Hamas.


Chanzo

VOA Swahili

Previous Post Next Post

No Thumbnail

News app yako bomba sasa unaweza idownload kwa kubonyeza batani ya download hapa ,