Trending

Sheikh Ponda akamatwa na jeshi la polisi 
DAR: Jeshi la Polisi Kanda Maalum linamshikilia Katibu wa Shura ya Maimamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda kwa tuhuma za kupanga maandamano bila kufuata taratibu za Kisheria, ambapo ilidaiwa yalipangwa kuanzia Viwanja vya Mnazi Mmoja hadi Manzese 

Akizungumza na JamiiForums, Kamanda wa Kanda hiyo, Jumanne Muliro amesema “Awali, tulimueleza (Ponda) kuhusu utaratibu kuwa anatakiwa kutoa taarifa kwa Mkuu wa Polisi Wilaya, hakufanya hivyo, tukaona anahamasisha mitandaoni na baadaye kukusanya watu. Baada ya mahojiano tutaangalia dhamana kwa mujibu wa Sheria.”
Ameongeza “Tunamhoji kinachoendelea na anatoa ushirikiano, kwani walitaka kuandamana kuhusu masuala ya vita inayoendelea Palestina, tukiruhusu hivyo na wengine pia watataka kuandamana kuhusu mataifa mengine. Baada ya mahojiano tutaangalia dhamana kwa mujibu wa Sheria.”

Chanzo
Jamii forum
Previous Post Next Post

No Thumbnail

News app yako bomba sasa unaweza idownload kwa kubonyeza batani ya download hapa ,